Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Aliyekuwa mwalimu wa shule ya Bridge International Academy Ujamaa, Changoma Abdalla na anayekabiliwa na makosa ya kukata sehemu za siri za mwanafunzi wa miaka saba aliachiliwa huru baada ya kufungwa kifungo cha maisha hapo awali.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, jaji Martin Muya  alisema amezingatia kuwa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa kesi hiyo hauambatani kamwe, hivyo basi hakuna uahakika wa aliyehusika na makaosa hayo.

“Licha ya kuwa uchunguzi wa damu iliyokuwa kwenye dawati la shule hiyo kuambatana na ile ilikuwa kwenye surale ya mtoto huyo, haimanishi na haionyeshi wazi ni nani aliyehusika katika ukataji wa mtoto huyo,” alisema Jaji Muya.

Changoma alionekana akitoa machozi ya furaha punde tu baada ya kusikia ameachiliwa huru.

Itakumbukwa kwamba mwalimu huyo, kupitia wakili wake Pascal Nabwana alikata rufaa ya kupinga kifungo hicho cha maisha kwa misingi kwamba hukumu hiyo haikufuata haki na usawa wa mteja wake.

Changoma Abdalla anadaiwa kumkata mtoto huyo sehemu zake za siri kutumia wembe mnamo Januari 21 mwaka 2013 katika shule hiyo ya Bridge Academy huko Likoni.

Itakumbukwa mtoto huyo aliiambia mahakama kuwa alilazimishwa kulala juu ya dawati na mwalimu huyo kisha akamkata kutumia wembe, jambo lililotiliwa shaka na jaji Muya.