Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke mmoja aliyefikishwa kwenye mahakama ya Nakuru siku ya Jumatano kwa kosa la kuuza pombe haramu aliwaacha wengi kinywa wazi baada yakulia alipotakiwa ajitetee.

Upande wa mashtaka ulisema kuwa mshtakiwa alipatikana akiuza pombe hiyo bila ya leseni mnamo tarehe Oktoba 20, 2015.

Mshtakiwa huyo, Josephine Nyamongo, aliyekiri makosa ya kuuza lita 15 za pombe haramu aina ya chang’aa, lita tatu za kang’ara na kwa kuuza pombe hiyo bila leseni, aliangua kilio huku akieleza mahakama kuwa pombe hiyo haikuwa yake.

Alifafanua kuwa hakuwa muuzaji bali alikuwa anachunga pombe hiyo ili apate malipo ya kumwezesha kugharamia matibabu ya mgonjwa anayeishi naye.

Hivyo basi, aliomba mahakama hiyo ya Nakuru kupitia kwa Hakimu mkuu Liz Gicheha imsamehe.

Kesi hiyo itatajwa tarehe Novemba 5 na kusikizwa tarehe Novemba 24, 2015.