Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamke anayedaiwa kumuibia mwajiri wake Sh100,000 alifikishwa kwenye mahakama moja ya Nakuru siku ya Jumatatu kujibu shtaka hilo.

Mshtakiwa, Jackline Cheragat, anadaiwa kumwibia mwajiri wake Jane Wanja, pesa hizo mnamo tarehe Agosti 5, 2015 katika duka moja la Mpesa lililo mjini Nakuru.

Hata hivyo, Cheragat alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu mkaazi Liz Gicheha, ambaye alimwachiliwa kwa bondi ya Sh80,000 au Sh50,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tarehe Oktoba 29, na kuskizwa tarehe Desemba 8, 2015.