Mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge katika eneo bunge la kitutu masaba kaunti ya Nyamira Victor Ogeto ameomba serikali kuinua kiwango cha hospitali ya Keroka kuwa ili kuwahudumia wagonjwa kwa kiwango kinachostahili.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumamosi kwa hafla ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa ya kiadventista ya Beyond Keroka Township, mwanasiasa huyo alisema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wengi, jambo ambalo linaleta msongamano mkubwa.

“Naomba serikali kujenga na kufungua wadi ambazo wagonjwa watalazwa ili huduma yao iweze kuifanywa ipasavyo,” alisema Ogeto.

“Ikiwa tunahitaji wagonjwa kuhudumiwa vyema katika hospitali ya Keroka sharti hospitali hiyo iongezewe madaktari pamoja na kupanuliwa ili huduma iweze kutolewa inavyostahili,” aliongeza Ogeto.

Wakati huo huo, wakaazi wa eneo hilo walionekana kufurahia ombi la mwanasiasa huyo na kusema kuwa jambo hillo likifanyika, basi huduma itakuwa ya kufurahisha katika hospitali hiyo.

“Tunahitaji hospitali ya keroka kubadilishwa jinsi mwanasiasa wetu amependekeza ili hata madaktari kuongezwa maana unapata wagonjwa wengi hutumwa katika hospitali ya Kisii na hiyo ni ishara ya kuonyesha huduma ambayo hutolewa katika hospitali ya Keroka si ya kutosha,” alihoji Kevin Osiemo, mkaazi.

Kwa hafla hiyo ya kuchangisha fedha, zaidi ya shillingi million mbili zilichangishwa.