Mwenyekiti wa manaibu gavanava nchini ambaye pia ni Naibu gavana wa kaunti ya Kisii Joash Maangi ameahidi kuwa serikali ya kaunti ya kisii itaendelea kusaidia shule zilizomo kwa kaunti hiyo ili kuinua viwango vya masomo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungungumza siku ya Jumamosi katika shule ya upili ya St Benedict kwa hafla ya kuzawadi wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, Maangi alisema serikali ya kaunti ya Kisii itahakikisha kuwa viwango vya elimu vimeinuka zaidi kwa kushirikiana na shule pamoja.

“Sisi kama serikali ya kisii tutajaribu tuwezalo, wanafunzi wa shule zilizoko katika kaunti hii wamepita katika mitihani yao maana tutaendelea kushirikiana nanyi ili shule za Kisii zifanye vyema kwa mitihani,” alisema Joash Maangi.

Aidha, naibu huyo alisema itakuwa vizuri zaidi sekta ya elimu kukabidhiwa serikali za kaunti maana ndizo ziko karibu na shule ikilinganishwa na serikali ya kitaifa.

“Tunaomba serikali ya kitaifa kuachilia sekta ya elimu kuwa katika serikali za kaunti kama njia mojawapo ya kuinua viwango vya masomo juu zaidi,” aliongeza Maangi.

“Kukarabatiwa kwa shule unastahili kufanywa na serikali za kauntim, ndio maana tunaomba tukabidhiwe hayo mamlaka ya kujenga shule zetu na sekta ya elimu itakuwa nzuri zaidi katika masomo,” alisisitiza.