Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Naibu Gavana wa kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo ametofautiana na gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama kuhusu uongozi wa kaunti.

Hii ni baada ya kubainika kuwa gavana Nyagarama yuko na nia ya kuwarudisha maafisa sita waliosimamishwa kazi kwa madai ya ufisadi katika kaunti, jambo ambalo halijawahi pata suluhu hadi sasa.

Akiongea na waandishi wa habari siku ya Jumatano mjini Nyamira, Nyaribo alikiri kuwa Nyagarama hajamjulisha lolote kuhusu nia hiyo ya kutaka maafisa hao kurudishwa kazini, ila alisikia hayo na kuyapata kupitia vyombo vya habari, jambo ambalo hakubaliani nalo.

Kamati iliyoundwa ya kuwachunguza maafisa hao sita waliosimamishwa kazi kwa madai ya ufisadi kwa kuvuja pesa za umma.

Wanne kati yao waliondolewa madai hayo ya ufisadi baada ya kamati iliyochaguliwa kuwachunguza kutoa ripoti kuwa hawana hatia, huku ripoti hiyo ikikataliwa vikali na kutupiliwa mbali na wawakilishi wa bunge la kaunti ya Nyamira.

“Mimi kama naibu wake hajanijulisha lolote kuhusu kurudishwa kazi kwa maafisa hao sita, na hata ninapoongea sina habari yoyote kuhusu nia hiyo lakini nasubiri nione ni lipi litakaloendelea,” alisema Nyaribo.