Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisii Joash Maangi amewaomba vijana kutoka Kaunti ya Kisii kutotumiwa na wanasiasa kuwatusi baadhi ya viongonzi.

Akizungumza mnamo siku ya Jumamosi katika mji wa Kisii, Naibu Gavana huyo Maangi aliomba vijana kufanya kazi ya kujiendeleza badala ya kutumiwa na wanasiasa ambo alisema hawasaidii hata.

Aidha, Maangi alikashifu vikali wanasiasa ambao wanawatumia vijana kutusi viongonzi na kuwaomba kukoma kufanya hivyo na kusema ni kukosa heshima miongoni mwao.

Maangi pia aliwaambia wanasiasa kuwa badala ya kuwaelimisha vijana kufanya hivyo ni vizuri wawatafutie vijana hao njia ya kujisaidia siku sijazo kama wanahitaji kujiendeleza kisiasa.

Wakati uo huo, Maangi alitumia fursa hiyo kuwaomba wanasiasa kutoka Kaunti ya Kisii kushirikiana na viongonzi walio mamlakani kufanya maendeleo katika eneo hilo na kutafuta njia ya kuwasaidia vijana hao ili nao waweze kujiendeleza kimaisha.

“Mwaka wa 2017 ni mbali sana, kwa sasa tuweke masuala ya siasa kando na tufanye maendeleo ili wananchi waweze kufaidika na tusonge mbele,” alisema Maangi, naibu gavana wa Kaunti ya Kisii.

Maangi aliongeza,  “Nawaomba vijana msidanganyike kamwe kutumiwa kuwatusi viongozi ambao wanahitaji kuwafanyia maendeleo maanake nyinyi ndio mtajipata kortini kwa kosa hili, bali sio wanaowatumia vibaya,” alionya Maangi.