Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kampuni ya maduka ya jumla ya Nakumatt inalenga kukusanya zaidi ya shilingi milioni 12 kuendeleza uhamasisho kuhusu ugonjwa wa saratani.

Mpango huo ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa saratani ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa kumi.

Kampuni hiyo inalenga kukusanya pesa hizo kupitia kwa wateja wao ambao hutumia kadi al maarufu 'Smartcard' kununua bidhaa katika matawi ya Nakumatt kote nchini.

Kupitia kwa mpango huo, wateja wa Nakumatt ambao wana kadi hizo watapata nafasi ya kukomboa pointi zao kupitia kwa kadi hizo, ambapo kila pointi itakauwa shilingi mbili.

Kila mteja wa Nakumatt ambaye ana kadi husika anatrajiwa kuchangia mradi huo shilingi mbili.

Zozezi hilo linaendeshwa kupitia ushirikiano kati ya Nakumatt na shirika la Faraja Trust Cancer Support.

Mkurugenzi shughuli na maswali ya ushirika katika kampuni ya Nakumatt Thiagarajan Ramamurthy alielezea matumaini ya kukusanya fedha lengwa.

“Katika mpango huu, tunalenga kukusanya zaidi ya shilingi milioni sita, fedha hizi zitasaidia kuendeleleza uhamasisho kuhusu saratani hasa mwezi huu wa kumi wa maadhimisho ya mwezi wa saratani,” alisema Ramamurthy.

Matawi yote 54 ya Nakumatt Afrika mashariki yanahusishwa katika shughuli hiyo.

Ramamurthy alisema mwaka jana mpango huo ulifanikishwa kukusanya shilingi tano milioni, ambazo zilitumika kusaidia wagonjwa wa saratani nchini.

Tawi la Nakumatt la Eldoret litaendeleza uchunguzi wa saratani katika tawi la maduka hayo la barabara ya Uganda kwa ushirikiano na kituo cha kushughulikia wagonjwa wa saratani cha Hospice.