Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Ndugu wawili wenye umri wa makamo walifikishwa kwenye mahakama moja ya Nakuru siku ya Jumatano kwa mashtaka mawili ya wizi.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama kuwa tarehe Oktoba 3, 2015 katika kata ndogo ya Piave, Njoro, Isaac Kiiru na Patrick Miiri wanadaiwa kuvunja na kuingia katika boma moja na kuiba jogoo 40, wenye thamani ya Sh40,000.

Katika shtaka la pili, wanadaiwa kuiba gunia la kilo 90 la mahindi na lingine la maharagwe, yenye thamani ya Sh6,500, mali ya Jeniffer Njoroge.

Hata hivyo, walikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Mkuu Joel Ng’eno.

Wawili hao waliachiliwa kwa dhamana ya Sh40,000 kila mmoja huku wakisubiri kesi hiyo kutajwa tarehe Oktoba 12, 2015 na kusikizwa tarehe Oktoba 15, 2015.