Seneta wa Kaunti ya Nyamira Kennedy Okong’o amemuomba waziri wa usalama wa ndani nchini Joseph Nkaissery kuongeza maafisa wa polisi mpakani Borabu Sotik ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
Akizungumza siku ya Jumapili mjini Nyamira, Okong’o alisema kuwa tayari amemuandikia waziri Nkaissery barua ya kumtaka kuongeza vituo vya polisi mpakani humo ili kuimarisha usalama kikamilifu.
“Ikiwa tunahitaji usalama katika mpaka huu wa sotik na Borabu, sharti maafisa wa polisi waongezwe ili uimarishaji wa usalama uweze kuafikiwa kikamilifu,” alisema Okon’go.
Aidha, Okong’o aliomba wakazi kushirikiana pamoja katika masuala ya usalama ili visa vya mauaji viweze kupungua katika eneo hilo.
Wizi wa ng’ombe umekuwa ukikithiri mpakani Borabu Sotik jambo ambalo limelazimisha waziri wa usalama Nkaissey kuombwa kuweka maafisa wa polisi mpakani humo ili kupunguza visa vya wizi katika eneo hilo.
Wakati huo huo, Seneta Okong’o aliomba Gavana wa Bomet Isaac Ruto na Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama kuja na kushirikiana pamoja kuhakikisha usalama umewekwa katika mpaka huo.
“Naomba magavana hawa wawili kuungana kutafuta mbinu ya kupunguza wizi na kudorora kwa usalama katika mpaka wa Borabu Sotik.