Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya kaunti ya Kisii imetenga asilimia 40 ya bageti ya mwaka wa elfu 2015-2016 katika sekta ya afya kama njia moja ya kuhakikisha kuwa sekta hiyo imeimarika na kuwasaidia wananchi wote.

Akiongea siku ya Jumanne katika wadi ya Tabaka eneo bunge la Mugirango Kusini, ambapo serikali ya kaunti ya Kisii kwa ushirikiano na sekta ya afya ilipeleka kliniki ya 'Beyong Zero', Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alisema kuwa bageti ya kaunti ya Kisii itatenga asilimia 40 ya bageti hiyo katika sekta afya ili kuinua viwango vya afya katika kaunti ya Kisii na viunga vyake.

“Asilimia 40 itashughulikia maswala ya afya ili tuhakikishe kuwa kila mwananchi amepata huduma bora ya afya," alsiema Gavana Ongwae.

Aidha, aliwaomba wakaazi wote katika kaunti ya Kisii kushirikiana ili kuinua viwango vya afya na kuwaomba wakaazi wa eneo bunge la Mugirango Kusini kijitokeza ili kupimwa katika kiliniki hiyo ambayo itakuwa huko kwa siku tatu ili kuwasaidia wakaazi hao.

Ongwae aliwaomba wakaazi hao kujitokeza ili kupimwa ugonjwa wa ukimwi kama njia moja ya kujua hali yao na kufanya kampeini ya kupunguza ugonjwa huo.

Kulingana na Gavana Ongwea, watu wakijitokeza na kujua hali yao ya afya, itakuwa njia moja ya kusaidia serikali ya kaunti kubaini idadi ya wale wameathirika ili waweze kusaidiwa na dawa na kupewa ushauri wa jinsi ya kuishi katika jamii.