Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Kisii imeweka mikakati ya kujenga daraja la Nyamache-Nyatira katika wadi ya Basi eneo bunge la Bobasi ili kuinua viwango vya uchukuzi katiki eneo hilo.

Akiongea na waandishi wa habari siku ya Jumanne, Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae alisema kuwa serikali yake imeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile barabara, hospitali, maji na elimu imetekelezwa. 

Ongwae alisema kuwa ameagiza maafisa wake wanaosimamia sekta ya ujenzi katika kaunti ya Kisii kuzuru eneo la Bobasi ili kuangalia mahala daraja hiyo itakapojengwa.

“Tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa Daraja hili imejengwa. Nimetuma maafisa katika sekta hiyo na wataangalia jinsi ujenzi unastahili kufanyika ndiposa tuweze kujenga daraja hilo," alsiema Gavana Ongwae.

Ongwae alisema kuwa hiyo ni njia mojawapo ya kuinua viwango vya uchukuzi katika Kaunti ya Kisii kwani kuna wafanyibiashara na watu wengine wanaohitaji kutumia daraja hilo na kama gavana wa kaunti hiyo atahakikisha kuwa amewasaidia wakazi wote. 

Alisema kuwa serikali yake itakarabati barabara katika Kaunti hiyo na kuwaomba wakazi wote kushirikiana na serikali ya kaunti ili miradi kama hiyo iweze kuendelea na kunawiri.

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwea amesema kuwa serikali ya kaunti imeweka mikakati ya Kujenga Daraja la Nyamache-Nyatira Picha Maktaba]