Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeiomba NEMA kuharakisha na kukubali ujenzi wa kituo cha magari katika eneo la Ogembo ambacho kaunti hiyo ilianzisha katika eneo hilo.

NEMA ilisimamisha shughuli ya ujenzi huo hapo awali huku wakiendelea na shughuli yao ya kawaida kabla ya ujenzi ukubaliwe.

Akiongea na Waandishi wa habari katika hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii wakati aliwatembelea manusura wa ajali iliyotokea katika eneo la Ogembo siku ya Jumapili, Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwea aliiomba NEMA kukubali ujenzi wa kituo hicho ili kuzuia maafa ya ajali ambayo yanashuhudiwa katika maeneo hayo kila wakati.

“Naomba NEMA kukubali ujenzi wa kituo cha magari katika eneo hilo la Ogembo kwa kuwa sisi kama serikali ya kaunti tupo tayari kujenga kituo hicho,” alihoji Gavana Ongwea.

Aidha, alisema kuwa serikali ya Kaunti ya Kisii wakishirikiana na idara ya barabara watahakikisha wameweka matuta katika barabara hilo ili kupunguza mwendo wa kasi wa magari na bodaboda katika eneo la Ogembo kwa kuwa mahali hapo kuna soko na wahudumu wa magari na waendeshaji bodaboda.