Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amesema kiwango cha ushuru kinachokusanywa katika kaunti hiyo kimerudi chini mno ikilinganishwa na siku za hapo mbeleni.

Akiongea siku ya Jumatano afisini mwake iliyoko mjini Kisii wakati chuo kikuu cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) kilikuwa kinatia sahihi na serikali ya kaunti hiyo, Gavana Ongwae alisema Kaunti ya Kisii inastahili kukusanya billioni moja kwa kila mwaka lakini kwa sasa haiwezi kukusanya hata nusu ya kiasi hicho.

Gavana Ongwae alisema hayo husababishwa na masuala ya kisiasa yanayoendelea katika kaunti hiyo.

Wakati huo huo, Gavana Ongwae aliomba chuo kikuu hicho kushirikaiana na serikaili yake ili kuhakikisha kuwa ushuru unaokusanywa kwa kaunti hiyo unakusanywa kwa njia ya teknologia ya kisasa ili kuafikia kiwango kile kinachohitajika.

“Ukusanyaji wa ushuru umeonekana kuhusishwa na mambo ya kisiasa katika kaunti hii jambo amabalo limepelekea ushuru kurudi chini mno,” alisema Gavana Ongwae.

Aliongezea: “Naomba chuo chetu cha JKUAT kushirikiana nasi ili ushuru ukusanywe kwa njia ya kidigitali kupitia teknologia ya kisasa ili tuone kama tutakusanya kiwango kile tumewekewa kuafikia. Katika Kaunti ya Kisii, tunastahili kukusanya billioni moja kwa kila mwaka lakini siku hizi hata kukusanya nusu ya pesa hizo ni vigumu sana kwani siasi imeingizwa katika ukusanyaji wa ushuru.”

Naibu chancellor wa chuo hicho cha JKUAT Bernard Otoki aliitikia wito wa gavana na kusema kuwa watahakikisha ushuru imekusanywa kwa njia ya kiteknologia ya kisasa.