Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Kitutu Chache ambaye pia ni mwanakamati wa tume ya bunge inayoshughulikia masuala ya fedha ameahidi kuona kuwa suala la mgomo wa walimu linashughulikiwa kwa haraka na hela kutafutwa ili kuwalipa walimu.

Mbunge huyo akiongea kwenye hafla iliyoandaliwa kwenye uga wa michezo wa Gusii siku ya Jumamosi kusherehekea miaka ishirini ya huduma ya Askofu mkuu wa dayosisi ya Kisii, Mairura Okemwa alisema kuwa sharti suala hilo lipewe heshima linalostahili.

Onyoka alimtaka spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi kukatiza likizo ya wabunge na kutumiwa barua warudi kwa dharura ya kujadili suala hilo la walimu kabla ya wanafunzi kuathirika zaidi, kwani kila mtoto wa kila mkenya na haki ya kupata elimu vile katiba ya Kenya inasema.

“Hili suala la mgomo limekuwa kero, sharti lishughulikiwe mara moja, ndio walimu wapate haki yao ili wanafunzi waweze kuenda shuleni kuendelea na masomo yao, maana hawa ambao wanaathirika zaidi ni wale ambao watafanya mtihani wa darasa la nane na wale wa kidato cha nne” alisema Onyonka.

Haya yanajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kudai kuwa yeye hana hela za kuwalipa walimu kwani wakiongezwa kila mfanyakazi wa idara za umma atataka kuongezewa mshahara, usemi ambao hakuwafurahisha wengi wakiwemo viongozi wa vyama vya kuwatetea walimu.

Katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini Bwana Francis Atwoli alitishia kuwaongoza wanachama wake kufanya maandamano ya kuwaunga walimu walipwa nyongeza yao ya mishahara vile korti iliamuru.