Huku baadhi ya vijana katika huduma kwa taifa wakifanya migomo kwa kutolipwa hela zao, vijana kutoka eneo bunge la Kitutu Chache wamehakikishiwa kuwa watalipwa hela zao katika muda ule watakuwa likozoni.
Haya yamethibitishwa na mbunge wa eneo hilo Richard Onyonka aliyekuwa akizungumza na vijana hao siku ya Jumatatu wakati wa kuangalia mafanikio wamefanya tangu waanze shughuli hiyo.
Vijana hao zaidi ya elfu moja ambao walipewa ruhusa rasmi na mbunge huyo kuenda kupumzika kwa muda wa wiki mbili walitolewa shaka kuwa pesa yao watapewa.
Onyonka alisema kuwa kwenye muda huo ambao watakuwa mapumzikoni, watakuwa wanapokea hela zao kwenye akaunti zao za mpesa, na akawataka wasiwe na shaka yeyote.
Aidha, alithibithisha kuwa aliongea na waziri wa maswala ya ugatuzi nchini Bi Ann Waiguru na akamtibitishia hayo.
“Japokuwa mnaenda kwenye likizo hii fupi ya wiki mbili, mkae mkijua kuwa kwenye siku hizo ambazo hamtakuwa kazini, mtakuwa mnapata kitu kwenye simu zenu, kwa vile niliongea na waziri wa ugatuzi hivyo msiwe na hofu yoyote,” mbunge huyo aliwahakikishia.
Aliwataka pia kuwa na nidhamu kama hiyo ambayo wameonyesha wakati huu wamekuwa wakifanya kazi na miradi ya kuboresha mji, ambapo aliwataka wengine ambao hawakupata nafasi kuajiriwa wakati wa kwanza kuwa tayari kwa nafasi ambazo zipo na kusema kuwa wataongeza vijana wengine kabla ya mwezi huu kukamilika.
Kiongozi huyo aliwapongeza wale wote walihudhuria hafla hiyo, na kuwataka wakazi kumuunga mkono kwenye miradi ya maendeleo.