Share news tips with us here at Hivisasa

Wazee wawili walijipata mashakani siku ya Jumamosi baada ya kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi baada ya kupatikana wamelewa chakari katika eneo la Makuli, Kaunti ndogo ya Matungulu, Machakos.

Chifu wa eneo la Tala, Pius Nzioka, akidhibitisha kisa hiki alisema kuwa wawili hao walikamatwa usiku wa manane na maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria.

Wawili hao waliokuwa wamelewa chakari kiasi cha kushindwa kutembea walipatikana wamejilaza kando ya njia kabla ya kutiwa pingu na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha Tala.

Chifu huyo alikashifu vikali kitendo hicho na kudai ni cha aibu mno kwani waliotakiwa kuonyesha mfano mwema kwa wananchi ndio walikuwa kwenye msitari was mbele kuwapotosha wananchi.

"Inasikitisha sana na kutamausha kuona viongozi wanaotarajiwa kuwa na mfano mwema wanaopaswa kuonyesha maadili mema ndio wavunja sheria," alisema Bw Nzioka.

"Ni vyema mkono was sheria umekumbana nao na hivyo sheria itafuata mkondo wake ili wawe funzo kwa viongozi wengine wenye nia ya kuwapotosha wananchi."

Washukiwa hawa waliojawa na haya nyusoni zao kwa sasa wanazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Tala huku wakisubiria kufikishwa kortini hapo siku ya Jumatatu.