Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maafisa wa polisi mjini Nyamira wameanzisha msako dhidi ya mwanamume anayeshukiwa kusababisha kifo cha mkewe.

Inadaiwa kuwa mwanamume huyo alimpa mkewe kichapo kwa kumshuku kulala na wanaume wengine.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Nyamira Ricoh Ngare, alisema kuwa mwanamume huyo, Bw Polycap Ongera, anadaiwa kumjeruhi mkewe kwa kumchapa akitumia kifaa butu, hali iliyomsababishia majeraha mwilini, na alipopelekwa kwenye hospitali kuu ya Nyamira, akaaga dunia.

"Mshukiwa wa mauaji tunaye msaka alimsababishia majeraha makali mkewe baada yakumchapa kwa kutumia kifaa butu na alipopelekwa hospitalini, akaaga dunia kutokana na majeraha hayo,” alisema Ngare.

Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hifadhi ya Hospitali Kuu ya Nyamira ukisubiri kufanyiwa upasuaji huku jamaa huyo akiwa mafichoni.