Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Balozi wa umoja wa mataifa al maarufu United Nations Habitat Profesa Sam Ongeri amewaomba vijana nchini kutojihusisha na masuala ya ndoa ya jinsia moja akisema ni kinyume na Mungu pamoja na utamaduni wa mwafrika.

Akizungumza siku ya Ijumaa katika Shule ya Upili ya Moi Gesusu iliyoko eneo bunge la Nyaribari Masaba, Kaunti ya Kisii wakati shule hiyo ilikuwa inasherehekea siku ya elimu, Profesa Ongeri aliwaomba vijana wote nchini kutokubali kufanya ndoa ya njisia moja kwa kusema ni njia moja ya kukandamiza kisasi kichacho ikiwa ndoa hiyo itakubaliwa nchini.

“Sisi kama Wakenya tumekataa hatutakubali ndoa hiyo ya jinsia moja kufanyika katika nchi yetu maana hatutakuwa na kisasi kingine ikiwa ndoa hiyo itakubaliwa humu nchini,” alidokeza Profesa Sam Ongeri.

“Naomba vijana kukataa ndoa hiyo sisi tunahitaji kuendelea kuona kila mtu akifuata yale yameandikwa katika bibilia takatifu kuwa mume anastahili kumuoa mke wala sio mwenzie,” aliongeza Profesa Ongeri.

Wakati uo huo, Profesa huyo aliwaomba vijana kutojiingiza na masuala ya kujiunga na vikundi vya kigaidi humu nchini maana vikundi hivyo hutekeleza uhalifu na kuomba kila mwananchi kuendelea kuombea nchi ya Kenya ambayo yaendelea kushambuliwa na kikundi cha Al-Shabaab.

“Mkisahau kuomba tutakuwa katika hali mbaya ya kupoteza maisha. Naomba tuendelee kuombeana na kuombea nchi yetu ya Kenya pamoja na nchi zingine ili uhalifu usije ukashuhudiwa nchini tena,” alisema Profesa Ongeri.

Aidha, Profesa Ongeri aliomba kila mtu kuwa na heshimu kwa wenzao na kujifundisha kuwa na tabia iliyo bora ili nchi ya Kenya iweze kuendelea mbele kimaendeleo.