Share news tips with us here at Hivisasa

Huku siku ya watoto ikiadhimishwa siku ya Jumapili kote ulimwenguni, mjini Mombasa wazazi wametakiwa kutowabagua watoto wa kike katika masomo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mjini Mombasa, Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar alisema wakati wa jamii kumchukulia mtoto wa kiume kuwa bora kuliko wa kike umepitwa na wakati.

Seneta Hassan vile vile aliwaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao ili iwe rahisi kwao kuwaeleza matatizo yanayowakumba.

Maneno yake yaliungwa mkono na mwakilishi wa wanawake Mombasa Mishi Mboko, aliyewakemea wanawake wanaoficha waume wao wanaowadhulumu kimapenzi watoto wa kike.

Alisisitiza haja ya kulindwa kwa watoto wa kike kwani wanapitia dhulma nyingi kuliko wale wa kiume.