Wizara ya Afya katika kaunti ya Mombasa imewahimiza waathirwa wa dawa za kulevya katika kaunti hiyo kujitokeza na kupata matibabu maalum.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Waziri wa Afya katika kaunti ya hiyo Binti Omar alisema kwamba mpango waliouzindua hivi majuzi wa kuwatibu waathiriwa wa mihadarati unalenga kuwanasuru vijana wadogo waliojitosa katika janga hilo.
Binti alisema kwamba waathiriwa hao watapewa tiba maalum aina ya kwa waraibu wa kujidunga sindano, huku waathiriwa dawa zingine wakipangiwa tiba zao kwani mpango huo unaolenga kuwaokoa vijana waliojitosa katika janga hilo.
“Mpango huu ulizinduliwa hivi majuzi kuwasaidia waathiriwa wa dawa za kulevya aina ya heroini kwa kujidunga sindano ndio watapata tiba ile ya Methodine tuliyoizindua. Na kwa wale wengine tuna mpango pia wa kuwasaidia kwa sababu wote ni vijana wetu," alisema Omar.
Aidha, ameihimiza jamii kujitokeza na kuwashsuria vijana kuenda katika vituo cha kuwarekebishia waraibu wa mihadarati tabia ili kupunguza idadi ya vijana wanaotumia mihadarati.
“Tafadhalini ndugu zangu tuwe tayari kujitokeza na kuwashauri vijana wetu kuvitembelea vituo vya kuwarekebishia tabia waraibu wa dawa za kelevya kwani idadi kubwa ya vijana katika kaunti yetu wameathirika,” alisema Omar.
Waziri huyo wa Afya vile vile ameahidi kuzuru mashinani na kuwahamsisha wakaazi jinsi ya kuwarai vijana wao walioathirika na mihadarati kujitokeza na kupata matibabu maalum.