Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wahudumu wa magari katika mji wa Ikonge, Kaunti ya Nyamira wameiomba serikali ya kaunti hiyo kuwatengenezea kituo cha magari katika eneo hilo.

Wakiongea siku ya Jumatatu na mwandishi huyu katika soko la Ikonge, wahudumu hoa walisema kuwa wamekuwa wakikumbwa na shida kubwa kwa ukosefu wa kituo cha magari.

Kwa sasa wameiomba serikali ya kaunti hiyo kuwashughulikia na kuwakarabatia kituo hicho kama njia mojowapo ya kuzuia ajali za kila mara zinazoshuhudiwa kati eneo hilo.

Haya yanajili baada ya magari aina ya matatu kugongana katika eneo hilo kwa sababu ya msongamano na ukosefu wa kituo cha kupangia.

“Tunaomba serikali yetu ya Nyamira kutukarabatia kituo cha magari na kuweka mipangilio katika soko hili, ili kukinga ajali hizi zinazosababishwa kila mara kwa sababu ya ukosefu wa kituo na utaratibu katika mahali hapa," alisema Daniel Nyabwasu, mhudumu wa matatu katika eneo hilo.

Hezron Borura, mwendeshaji wa bobadoda alisema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na kituo katika eneo hilo kwani wamekuwa wakiomba kituo hicho kwa muda sasa lakini serikali bado haijasikia kilio hicho.

Walisema ni muhimu kilio hicho kusikizwa na kutekelezwa ili kunufaisha wahudumu na wafanyibiashara kwa jumla.

Jambo hilo liliungwa mkono na baadhi ya wafanyibiashara katika soko hilo kwa kusema kuwa kituo hicho kitakuwa na faida kumbwa kwao haswa kwa kuinua biashara zao.