Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kutumia pesa za wananchi vizuri kwa kufanya maendeleo kikamilifu.
Akiongea siku ya Jumatatu mjini Kisii, Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kusini, Manson Nyamweya, alisema kuwa serikali ya Kaunti ya Kisii tayari imepokezwa mabillioni ya pesa ambazo zinastahili kufanya maendeleo ili wananchi wa kauntii hiyo kufurahia uongozi uliopo wa serikali za ugatuzi.
Mbunge huyo alisema pesa ambazo serikali hiyo hupokezwa zinastahili kufanya maendeleo kwa maeneo bunge yote tisa yalioko katika hiyo.
Mbuge huyo alisema ziara zote za viongozi wa kaunti hiyo haziwezi msaidia mwananchi wa kawaida, ila mwananchi alichagua kiongozi atakaye mletea maendeleo.
“Naomba serikali ya Kaunti ya Kisii ijaribu kila iwezalo kwa kuleta maendeleo haswa kwa kukarabati barabara kikamilifu, kuweka miradi ya maji na mengine mengi ambayo yanaweza leta manufaa kwa wananchi wa kaunti hii,” alisema Nyamweya.
Aliongezea, “Mambo ya viongozi kuandaa vikao na kuenda ziara mbalimbali hayawezi kutusaidia. Yale tunahitaji kuona sisi ni maendeleo katika kila eneo bunge lililoko kwa kaunti ya Kisii.”
Aidha, Nyamweya aliomba serikali ya kaunti hiyo kuwalipa wanakandarasi wote kwa kazi zile ambazo wazimefanya katika kaunti hiyo.