Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imetenga Sh50m ili kupambana na mvua ya El Nino inayotarajiwa kunyesha kwanzia mwezi wa Oktoba hadi mwezi wa Disemba.

Hii ni baada ya kubainika kuwa mvua inayotarajiwa kuanza kunyesha itakuwa kubwa zaidi jambo ambalo lililazimisha serikali ya kaunti hiyo kutenga kitita hicho cha pesa ili kupambana na madhara ambayo yanaweza kutokea mvua hiyo itakapoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi mjini Kisii, afisa mkuu wa Idara ya kilimo katika kaunti ya Kisii Samuel Mogeni alisema kuwa serikali ya kaunti imetenga Sh50m ya kujitayarisha vyema ili kupambana na mvua hiyo nzito.

Aidha, aliomba wakazi wa kaunti ya Kisii kutengeneza mabomba wanamoishi ili maji ya mvua yasije yakawa mengi na kuharibu bidhaa zao kwa kuenda hadi kwa nyumba.

Mogeni alisema miongoni mwa sehemu ambazo huenda zikaathirika zaidi katika kaunti ya Kisii ni eneo la Bobasi, Mugirango kusini na Itumbe.

“Kama serikali ya kaunti tumetenga Sh50 ili tukabiliane na mvua hiyo ya El Nino. Naomba pia wananchi wa kaunti ya Kisii watengeneze mabomba ili maji hayo yasisababishe madhara mengi,” alisema Mogeni.