Kamishna wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi amesema vijana wa huduma ya NYS watalipwa vizuri baada ya usajili wa huduma hiyo kuendelea kutekelezwa katika maeneo bunge yote hapa nchini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza mnamo siku ya Jumatano katika uwanja wa shule ya upili ya Mosocho iliyoko eneo bunge la Kitutu Chache wakati vijana wa huduma ya NYS walikuwa wakisajiliwa, kamishna huyo alisema vijana hao watalipwa vizuri baada ya kuchaguliwa katika huduma hiyo.

Mradi huo wa usajili ulianza hapo jana, siku ya Jumatano ambapo vijana 1,300 wanatarajia kupata ajira hiyo katika eneo bunge la Kitutu chache kusini kaunti ya Kisii.

“Mradi huu ni mzuri na tunasema ni vizuri vijana wetu kupata mahala pa kufanya kazi katika nchi hii ya Kenya ambayo watajiendeleza kimaisha kupitia mradi huu wa NYS,” alisema Mwangi.

Kamishna huyo aliomba viongonzi wote kushirikiana na kufanya kazi pamoja ili nchi ya Kenya iendelee mbele.

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae, ambaye alitarajiwa kuhudhuria usajili huo alituma ripoti yake kuwa serikali ya kaunti itaendelea kuunga mkono mradi huo kwa njia moja au nyingine, huku akisema vijana ambao watachaguliwa watasaidiwa na serikali ya kaunti hiyo ya Kisii.