Share news tips with us here at Hivisasa

Wanabiashara wa soko ya Nyacheki lililoko eneo bunge la Bobasi kaunti ya Kisii wameomba serikali ya kaunti kuwaajiri watu wa kufanya usafi katika soko hilo na kutunza mazingira.

Hii ni baada ya wafanyabiashara kulalamikia hali ya usafi wa soko hilo, huku wakisema kuwa limechafuka kupita kiasi na bomba za kupitisha maji zikiziba na kusababisha harufu mbaya kwani maji machafu hayapiti.

Wakizungumza na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumanne katika soko hilo, wanabiashara hao wakiongozwa na Alice Mokaya walisema wanahitaji usaidizi kutoka kwa serikali ya kaunti ili kuishughulikia soko hilo kila wakati kama soko zingine.

“Tunaomba gavana Ongwae awaajiri watu wa kufanya usafi katika soko hili kwani tunavumilia harufu mbaya ambayo inaweza kutuathiri kiafya,” alihoji Rose Omanga, mwanabiashara.

Wakati huo huo, wanabiashara hao walisema kuwa ikiwa serikali haitafanya hivyo iwajulishe ili watengeneze kikundi ambacho kitakuwa kikilipa na ambacho kitafanya usafi huo na ushuru usikuanywe kwani pesa hizo hazifanyi kazi.

“Kila siku ya soko huwa tunatozwa ushuru, hizi pesa huenda wapi? maana zinastahili kukarabati soko na kufanya masuala ya usafi kwani zinatoka kutoka kwetu sisi wanabiashara,” alisema Cleophas Mosioma, mwanabiahara mwingine