Wakaazi wa wadi ya Tabaka eneo bunge la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii wameiomba serikali ya kaunti kukarabati soko la Tabaka .
Wakiongea hii leo, Alhamisi katika soko hilo, wafanyibiashara wa soko hilo wameiomba serikali kuwakarabatia soko hilo na kuweka vibanda ili kuwarahisishia biashara yao.
Aidha, walisema kuwa wakikarabatiwa soko hilo wataweza kuendeleza biashara zao kwa njia mwafaka, kwani huwa wanasumbuka sana haswa wakati wa mvu na jua kali kutokana na ukosefu wa vibanda .
“Naomba serikali ya kaunti ya Kisii kutusaidia kutukarabatia soko hili ambalo ni la msaada mkubwa kwetu na wafanyikazi wengine katika mahali hapa kwani hakuna soko lingine karibu hapa,” alihoji Calvin Onyoni, mfanyibiashara.
Kwingineko, wafanyabiashara hao wamepongeza serikali ya kaunti kwa kuweka mataa katika soko hilo, na kuomba ikarabatiwe zaidi ili kuimarisha usalama.
“Napongeza serikali ya kaunti kwa kuweka mataa haya katika soko hili na tunaomba vibanda ili tuweza kufanya biashara hata wakati wa usiku,” alihoji Grace Nyachama, mama mboga katika soko hilo.
Kwingineko wamewaomba wakazi wengine wanaojenga nyumba karibui na soko hilo kujua kuwa shamba hilo ni la soko, na wala si la mtu binafsi.