Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kuwasaidia wafanyibiashara wa jua kali mjini Kisii ili kuimarisha sekta hiyo .
Wito huo umetolewa baada ya kugunduliwa kuwa ni vigumu sekta hiyo kuinuka bila kushikwa mkono na serikali .
Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne mjini Kisii, mwenyekiti wa sekta hiyo mjini humo Fred Mainga, pamoja na wafanyibiashara wengine walisema sekta ya jua kali ni mojawapo ya nguzo mhimu sana nchini katika kuhakikisha kuwa kazi zapatikana kwa vijana ili kujiendeleza.
Kulingana na mwenyekiti huyo, sekta hiyo inasaidia serikali kutogharamika zaidi kwa kuagiza bidhaa flani kutoka nchi za ng’ambo, ilhali sekta hiyo hutengeneza bidhaa nchini katika kaunti mbalimbali hasa katika miji mikuu.
"Tunaomba gavana wa kaunti James Ongwae akumbuke sekta hii ili tujiimarishe kimaisha na tuinue uchumi wa kaunti,” alisema Mainga.
“Tunaomba serikali itusaidie kununua fanicha zetu na bidhaa zinginezo ambazo sisi hutengeneza na pia kuleta wawekezaji watakaotegemea wana jua kali katika shughuli zetu,” alihoji Daniel Ochoke, mmoja wa wanajuakali.
Pia wafanyibiahara hao wameomba serikali, kupitia idara ya biashara kuhakikisha kuwa hawasumbuliwi na askari wa kaunti ambao ili kuinua sekta hiyo.
“Vile tunajali serikali yetu, nayo pia ishuglikie masilahi yetu ili tuweze kujenga uchumi wetu pamoja na iagize askari hawa ambao wanatusumbua wakome kufanya hivyo,” aliongeza Mainga.