Serikali ya kitaifa imeombwa kutochelewesha vitambulisho na kadi za vitambulisho, ili kupata fursa ya kupiga kura na kuwachagua viongonzi wao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea mnamo siku ya Jumatatu katika mji wa Keroka ulioko eneo bunge la Kitutu Masaba, mwanasiasa aliyewania kiti cha ubunge Victor Ogeto alisema kucheleweshwa kwa vitambulisho huchangia viongonzi wengi wasiopendwa na Wananchi kuchaguliwa, na kuomba serikali kuu kufanya halahala na kuachilia vitambulisho haraka pindi wakenya wanapojiandikisha.

“Watu wengi hawapati nafasi ya kuchagua viongonzi wao maana hukosa vitambulisho baada ya kujiandikisha na tunaomba serikali kuu kerekebisha katika sekta hiyo,”alisema Victo Ogeto mwanasiasa.

“Viongonzi wengi huchaguliwa kinyume na matarajio ya wakenya wengine maana wakenya hao hawakupata fursa ya kupiga kura kwa kukosa kadi za kupiga kura,” aliongezea Ogeto.

Kwa upande mwingine, wakaazi wa eneo hilo walionekana kuunga mkono matamshi ya mwanasiasa huyo, huku wengi wakisema huwa wanajiandikisha kwa kupata vitambulisho lakini vinacheleweshwa kuwafikia.

“Mimi nilijiandikisha ili nipate kitambulisho mwaka wa 2012 mwezi wa tatu, nikaongojea mpaka kura zikafika sikuwa na kitambulisho, na hicho kitambulisho nilienda kukifwatilia na nilikipata mwezi wa sita mwaka wa 2013 baada ya uchaguzi kukamilika,” alihoji Samson Nyabengi, mkaazi wa eneo hilo.

“Mimi kuna mtu nahitaji kuchagua lakini hakupita, huenda hiyo kura yangu ingesaidia achaguliwe maana sikukipata kitambulisho kabla ya uchaguzi, ingawa nilijiandikisha mapema,” alisema Bosire Cliford, mkaazi mwingine.