Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kasisi wa kanisa ya Kisii katoliki, Lawrence Nyaanga, ameomba Serikali ya kitaifa kuamrisha walimu wakuu wa shule mbalimbali nchini kutoruhusu masomo kuendelea wakati wa wikendi ili wanafunzi kupata nafasi ya kuabudu Mungu.

Akizungumza siku ya Jumapili katika kanisa hiyo ilioko mjini Kisii, kasisi huyo alisema wanafunzi wengi hawaabudu kwa sababu wanasoma wakati wa wikendi.

Nyaanga alisema shule huchukua muda mwingi kuwasomesha watoto badala ya kuwapa wanafunzi wakati wa kuabudu. 

“Jambo ambalo limesababisha wanafunzi wengi kujiunga na vikundi vha majambazi na kujiunga na utumizi wa madawa ya kulevya ni kutopata fursa ya kuabudu Mungu. Wanafunzi husomeshwa hata wikendi na hiyo huwafanya kutojua mungu,” alisema kasisi Nyaanga. 

“Naomba serikali kuingilia kati suala hilo na kuamrisha walimu wakuu kutoruhusu masomo wakati wa wikendi ili wanafunzi wapate muda wa kuabudu,” aliongeza Nyaanga.

Wakati huo huo, kasisi huyo aliomba wazazi, walimu na wanafunzi kuchukua muda wao kuabudu Mungu na kusema masomo bila Mungu ni hasara maana hayawezi kupata mafanikio kamwe.

“Kila ofisi ya serikali hufungwa wakati wa wikendi kumanisha kuna umuhimu wa ofisi kufungwa wakati wa wikendi na kuruhusu watu kuabundu Mungu,” alisisistiza Nyaanga.

Kasisi huyo alisema kuwa sasa ni jukumu la serikali kuu kusikia kilio hicho ili wanafunzi wawezekupata muda wao kuabudu Mungu kila wikendi kama njia mojawapo ya kuzuia vijana wa nchi hii kujihusisha na utumizi wa madawa ya kulevya pamoja na masuala ya ujambazi.