Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu mkuu wa shule ya Upili ya Matutu PAG Charles Osoro amempongeza mwanasiasa victor Ogeto kwa kusaidia shule hiyo na kemikali za kutumika katika maabara.

Akiongea afisini mwake na mwaadishi huyu hii leo Jumanne, Osoro alimpongeza Ogeto kwa kusaidia shule hiyo, huku akiwaomba wanasiasa wengine kuiga mfano huo na kusaidia shule katika eneo hilo.

“Nampongeza Ogeto kwa msaada wake, na hii ni njia moja ya kuinua viwango vya masomo kati shule hii nasi tutahakikisha kuwa tutatumia vifaa hivyo ili kuinua alama zetu katika mtihani wa mwaka huu,” alihoji Osoro.

Aidha, alimpongeza mwanasiasa huyo kwa kujitolea kusaidia kuinua viwango vya masomo katika eneo hilo, haswa katika mradi wake wa kuwasaidia mayatima.

Mwalimu huyu alisema kuwa kemikali hizo, zinagharimu zaidi ya shillingi nusu million, zitawasaidia wanafunzi kufanya mazoezi na kufahamu vyema mambo ya chemia na bayologia.

Kwingineko, Osoro amewaomba viongozi walio mamlakani kwa sasa kupea masomo nafasi ya kwanza, huku akiomba serikali ya kaunti ya Nyamira Kutenga pesa zaidi katika sekta ya elimu.