Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Licha ya mahakama ya kushughulikia masuala ya wafanyakazi kuamrisha walimu wasitisha mgomo na kurudi shuleni, bado shule nyingi zimebaki mahame kwenye kaunti ya Kisii.

Uchunguzi wa huyu mwanahabari kwenye baadhi ya shule za umma umebainisha kuwa hamkua na wanafunzi wala walimu kwenye shule husika katika kaunti ya Kisii, huku ikiwa tu ni baadhi ya wanafunzi hasa wa kidato cha nne na wale wa darasa la nane ambao walikuwa wakiingia ijapo bila sare za shule.

Ben Onchoke, mmoja wa mzazi ambaye aliongea na mwandishi huyu kwenye lango kuu la kuingia katika shule ya msingi ya Jogoo, alisema kuwa bado hawajakuwa na imani kurudisha watoto wao shuleni sababu wengi wa walimu walishahapa kuwa hawatarudi shuleni mpaka walipwe.

“Mimi bado watoto wangu wawili wako katika shule za upili na sina hakika ni lini nitawarudisha shule, mpaka nisikie kutoka kwa viongozi wa Knut na Kuppet ndio niweze kuwapeleka wanangu shuleni, na ninaomba serikali iwe na huruma kwa wazazi kwani wengine wetu tulishalipa karo,” alilalama mzazi huyo.

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya upili ya Nyankongo ambao walizungumaza na huyu mwandishi walisema kuwa bado wanaendelea na masomo yao, na wakatoa matumaini yao kuwa watapita kwenye mtihani wa taifa ambao wanatarajia kuanza mwezi ujao.

Hata hivyo, walimu pamoja na wanafunzi katika shule za binafsi walikuwa wanaendelea masomo yao kama kawaida.