Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Bwana Keriako Tobiko ameagiza faili ya kesi ya gavana wa Kaunti ya Mombasa kurejelewa tena na kufanyiwa utathmini zadi kuhusiana na madai yanayomsonga.

Gavana Hassan Joho anadaiwa kuhusiana na kuuzwa kwa sehemu ya ardhi ya Soko la Mwembe Tayari iliyoko katikati ya mji wa Mombasa kwa mwekezaji wa binafsi.

Taarifa zilizowasilishwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi, kutoka afisi ya Tobiko zilisema kuwa sharti faili za kesi tatu husika ziangaliwe tena ili kuondoa shaka miongoni mwa raia ambao ndio waathiriwa kwenye kesi hizo.

Gavana Joho aliyakana madai hayo hapo awali ambapo alisema kuwa kipande hicho kinadaiwa kuuzwa hata kabla ya yeye kuingia kwenye uongozi wowote wa siasa kwenye miaka ya tisini.

Kesi hiyo iliweza kukosa ushahidi kulingana na Tume ya EACC na faili ya kesi hiyo kusimamishwa kuendelea, ambapo mapema mwezi huu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko aliagiza kufungwa kwa faili hiyo.