Serikali ya kaunti ya Kisii, kupitia msimamizi mkuu wa matibabu Bi Sarah Omache, imejitokeza na kusema kuwa lengo lao ni kutoa chanjo kwa idadi kubwa ya watoto walio chini za miaka mitano.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza katika hospitali kuu ya Kisii mnamo siku ya Jumatatu Omache alisisitiza leongo la serikali kuchanja idadi kubwa wawezavyo.

“Lengo letu wakati huu ni kutoa chanjo kwa watoto 292,490 kwa kampeini hii, pia tumepokea dosi 325,280 kutoka kwa serikali kuu,” alisema Omache.

Vilevile, afisa huyo alisema kwamba hakujakuwa na pingamizi yoyote kutoka kwa wazazi na wahisani kwa kuwasilisha watoto wao ili kupata dosi hiyo ya polio.

Aliwarai wazazi na wahisani kushirikiana na maafisa ili kukinga magonjwa mbalimbali, na pia kufikia idadi wanayoilenga.

Pia alifutilia mbali uvumi kutoka kanisa la katoliki unaolenga kuwazuia watoto kupata chanjo hiyo.

“Polio ni ugonjwa wa kawaida kwa watoto, unaweza kusababisha kupooza na pia kuleta madhara hatari, kwa hivyo futilia dhana mbaya zinazoenezwa kuhusu chanjo hii,” aliongeza Omache.

Kampeini hii ilianza Jumamosi, tarehe moja na itakamilika Jumatano tarehe tano.