Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu mkuu wa Shule ya Upili ya Wavulana St Patrick Nyabigena iliyoko eneo bunge la Mugirango Kusini, amewataka jamii ya Gusii kutunza mtoto wa kiume kuhakikisha hawajajihusisha na uhalifu katika jamii.

Akiongea katika shule hiyo katika hafla ya kujadili masuala ya elimu, mwalimu Yusuf Obare alidai kuwa watoto wa kiume wameachiliwa kufanya maamuzi, hali ambayo alisema isipoangaliwa vizuri itachangia watoto hao kuhisi upweke na kuanza vitendo vya uhalifu.

Obare aliwasihi wazazi, walezi na jamii kwa jumla kuweka usawa kwa watoto wao ili tusije tukawaacha jangwani.

Alisema kuwa mara nyingi watoto wa kiume ujihusisha na unywaji pombe na matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu ya kutengwa na kujichukia, hali ambayo alisema imechangia mno visa vya kuwaibia watu na ujambazi katika jamii.

Aidha, aliwataka viongozi wa kisiasa kuonyesha uongozi mwema kwa kuwashirikisha vijana wote kwa jumla katika masuala ya uongozi na kuanzisha ufadhili wa masuala ya michezo mabalimbali kama njia ya kuwawajibisha, hasa vijana wa kiume ili kuweka mawazo yao katika hali nzuri ambapo alisema kuwa kupitia michezo na shughuli za kazi huwaepusha vijana kuwa na mawazo mabaya.

Aliahidi kushirikiana na wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo hata na wale kutoka nje ya shule hiyo kuona wanainua maisha ya watoto wote kwa jumla ili wawe watu wa heshima kwa sasa na katika maisha ya baadaye.