Walimu wa shule za msingi wameombwa kuwa pamoja kila wakati haswa katika mashidano mbalimbali ili kutoa motisha kwa wanafunzi wao.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea na walimu na wanafunzi hii leo Jumanne katika hafla ya mashidano ya tamasha katika shule ya msingi ya Kisii, mwenyekiti wa Kepssa Julius Onyando aliwaomba walimu kushirikiana na wanafunzi ili kuinua michezo mbalimbali katoka kaunti ya Kisii

“Naomba walimu wanzangu kuwa vielelezo wema kwa wanafunzi na kuwapea wanafunzi motisha ili waweze kujiendeleza katika taaluma mbalimbali,” alihoji Onyado

Kwingineko walimu waliokuwa katika hafla hiyo iliyokuwa kwa siku ya pili na itakayokamilika kesho Jumatano walisema kuwa wako tayari kila wakati kushirikiana na wanafunzi wao.

Haya yote yanajiri wakati walimu waliwafurahisha mashabiki katika hafla ya mashidano ya kitaifa yaliyofanyika wikendi katika uwanja wa chuo cha Kisii baada ya kukimbia mbele ya wanafunzi .

“Nimefurahishwa na walimu hawa kwa ushirikiano wao mwema na watoto wetu na ninaomba kuwa wawe wanashirikiana kila wakati,” alihoji Dodwel Ombiro, Mzazi.

Mashidano hayo ya tamasha yalijumuisha shule zote za kibnafsi na shule za serikali ambayo yatakamilika hiyo kesho jumatano na watakaufuzu wataenda kuwakilisha kaunti ya Kisii katika kitengo cha Eneo mjini Migori