Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Machifu watatu wamelalamikia kile wamekitaja kuwa vijana ndio walio katika mstari wa mbele katika biashara ya kugema na kuuza pombe ya chang'aa katika Wadi ya Gesusu, Kaunti ya Kisii.

Wakiongea kwenye Baraza moja katika eneo la Nyamesocho siku ya Jumanne walipowanasa vijana wakiwa na pombe lita 20 ya aina ya chang'aa, chifu Thomas Nyansimerawa wa Mesabisabi, chifu Orina Ondicho wa Nyamesocho na chifu Machogu Nyauma wa Raganga, chifu nyansimera walisema kuwa Raisi wa taifa anawatakia vijana mema alipoagiza msako na kuangamiza pombe haramu nchini.

"Raisi anawatakia vijana mema lakini vijana walio na sikio ndio hatuna katika maeneo yetu na tunashangaa twaelekea wapi kama vijana ndio wapo katika mstari wa mbele katika biashara ya pombe haramu katika eneo hili," alidai chifu Nyasimera.

Aidha chifu wa Raganga bwana Nyauma amewataka vijana kujiunga na makundi ya kimaendeleo na yale ya taifa kama huduma ya vijana nchini al maarufu NYS ili wajipe nafasi ya kijikimu kutokana na ustadi watakao pewa na mafundisho.

Pia Nyauma aliotoa onyo kali kwa wakazi hao kutofanya aina yeyote ya biashara licha ya pombe akiwakumbusha kuwa ni agizo la raisi wa nchi wala sio la machifu wenzio.

Chifu Ondicho pia ameonya vijana na akina mama wa eneo lake ambao bado wanashiriki au wanaendeleza biashara hiyo na kuwasihi kukoma.

"Nawahurumia wale mtakao patikana aidha wakitengeneza, safirisha au wakiuza na pia wale wanaokunywa maanake hawatasita kuwapeleka katika vituo vya Polisi," alisema chifu Ondicho.

Kijana mmoja aliyefaamika kama Lukas Elijah alinaswa na lita 20 ya chang'aa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Ramasha akitegea kupelekwa kotini kwa shtaka la kusafirisha na kuuza chang'aa.