Vijana wanaoacha shule na kujiunga na uendeshaji wa bobaboda katika lokesheni ya Mochenwa, wadi ya Gesima wameonywa huku wazazi wao wakiombwa kuwarudisha shuleni.
Akiongea siku ya Jumatatu na mwadishi huyu, Chifu wa lokesheni ya Mochenwa Magara Makori alisema kuwa viwango vya vijana wanaoacha shule na kujiunga na sekta hiyo vimeongezeka pakubwa.
“Kuna vijana wengi ambao wanastahili kuwa shuleni lakini kwa sasa wamejiunga katika sekta hiyo licha ya kuwa shuleni ili waweze kupata mafunzo yatakayowasaidia siku zijazo,” alisema Magara.
Kwa sasa Magara amewaomba wazazi wa vijana hao kuhakikisha kuwa vijana hao, haswa wa umri wa kuwa shuleni, wamerudi ili kujiendeleza na masomo ambayo yatawasaidia katika siku zijazo.
Aidha, alisema kuacha shule kwa vijana hao ndio imechangia uhalifu katika lokesheni hiyo, jambo ambalo amesema kuwa yeye na afisi yake wameweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wamekabiliana vilivyo ili kukomesha visa hivyo.
“Sisi kama maafisa wa utawala tumeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa kila kijana ambaye anafaa kuwa shuleni anaende na tunahitaji ushirikiano wa wazazi ili kufanikisha hayo yote,” aliongezea Magara.
Kwingineko, alisema kuwa vijana hao wadogo wanapojiunga na sekta ya bodaboda, wengi wao huwa hawafahamu masharti ya barabara, ndiposa hukumbwa na ajali za kila siku, jambo ambolo linastahili kuchunguzwa.
Wazazi pia wameombwa kushirikina na washikadhaiu wa elimnu ili kuhakikisha kuwa wanao wanaenda shule kwa faida ya siku za zijazo.