Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana wengi kutoka eneo Bunge la Mugirango Kusini katika Kaunti ya Kisii walisusia kupimwa ugonjwa wa ukimwi ili kujua hali yao.

Akizungumza na Mwandishi huyu wa habari siku ya Jumanne katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Tabaka ilioko eneo bunge hilo kwenye shughuli hiyo iliyokuwa inatekelezwa, daktari aliyesimamia shughuli hiyo Simon Ayico alisema vijana walisusia kupimwa ili kujua hali yao huku wachache tu wakiitikia kushiriki zoezi hilo.

Nia ya kupimwa kwa wakazi wote wa eneo bunge hilo ulitekelezwa Jumanne huku shughuli hiyo ikiandaliwa na Serikali ya Kaunti ya Kisii kupitia mradi wa Beyond Zero Campaign.

Waliojitokeza ni akina mama pamoja na wazee, idadi iliyokuwa 345 kufikia mwendo wa saa 11:00 jioni huku vijana wakisusia kupimwa ili kujua hali zao jambo ambalo daktari aliyesimamia shughuli hiyo Simon Ayico kushindwa kulizungumzia.

“Ni vizuri vijana wetu kujua hali yao ili ikiwezekana kama tayari wameathirika wapewe maelezo kuhusu jinsi wataishi kwa muda mrefu, lakini leo wazee na akina mama ndio walijitokeza kupimwa, na tayari imeonekana kuwa vijana wa eneo hili wanaogopa kujua hali yao,” alisema daktari Ayico.

Wakazi wote wa Kaunti ya Kisii wameombwa kujihadhari sana na kulinda maisha yao ili wasije wakaathirika na ugonjwa huo ili kuendelea na maisha yaliyo bora hayo ni kwa mujibu wa Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ambaye alihudhuria shughuli hiyo.