Aliyekuwa naibu waziri katika serikali ya muungano iliyopita Musalia Mudavadi amewashinikiza viongozi wa kidini wale wakiislam na kikristu kuungana na kuhubiri amani miongoni mwa jamii ili taifa hili kuwa salama.
Akizungumza na wanabahari baada ya kukutana na viongozi hao mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Mudavadi alisema kwamba ni wakati sasa wa viongozi hao kuja karibu na kushirikiana katika kuhubiri amani ili kuwawezesha vijana kujinasua katika makundi ya kihalifu.
Mudavidi alisema kwamba jamii ya wapwani na Mombasa kwa jumla itafanikiwa kusitisha uhalifu na kuwazuia vijana katika kushawishi vibaya na baadhi ya watu fulani kuvuruga usalama wa eneo hilo iwapo viongozi wa kidini watajitokeza waziwazi na kuwaelimisha vijana kuhusu umuhimu wa maadili mema na jinsi dini inavyoangazia.
"Tumekutana leo na viongozi wa dini ya kiislamu baada ya kukutuna wa wale wa kikristu, tumejadilina mengi na tungependa kuwaambia ndugu zetu wazidi kudumisha amani na pia kuhubiri uiano na utangamano ili tuweze kuishi kwa amani kwa kushirikiana kama jamii moja kwa sababu sote ni wakenya na sio vizuri tukianza kubaguana kwa misingi ya kidini," alisema Mudavadi.
Mudavadi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha Amani aliwaonya viongozi wa kidini dhidi ya kujihusisha na siasa za uchechezi na kuangazia maswala muhimu ikiwemo ya kidini na amani ili kuliunganisha taifa hilo pamoja.
Kiongozi huyo ameahidi kuzuru kaunti zote nchini kukutana na viongozi wa kidini na kujadiliana jinsi ya kuwaunganisha vijana na jamii kwa jumla na kueneza amani kote nchini ili kuona kwamba idadi kubwa ya vijana wanaojitosa katika mswala ya uhalifu na ugaidi wanaokolewa na kuwalinda vijana.