Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Viongozi wote wa kaunti ya Nyamira wameapa kufanya kazi pamoja na gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama.

Hii ni baada ya Nyagarama kuonyesha uwazi kwa kutowaruhusu maafisa wake sita wa wizara mbalimbali kuendelea kuhudumu afisini kwa kudaiwa kuhusika na ufisadi ya zaidi ya shillingi millioni 100

Mnamo siku ya Alhamisi, gavana Nyagarama aliwasimamisha kazi sita hao, jambo ambalo limewapelekea viongozi wa kaunti hiyo kuahidi kufanya kazi na serikali ya kaunti kwa upamoja.

Wakiongea siku ya Jumapili katika sherehe ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kanisa ya katholiki ya Riakoroko iliyoko eneo bunge la Kitutu Masaba, wabunge wote katika kaunti ya Nyamira waliahidi kushikana mikono na gavana kuliendesha gurudumu la kaunti hiyo kimaendeleo.

Miongoni mwa wale waliosema wataungana na gavana Nyagarama ni mbunge wa mugirango magharibi James Gesami, mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire, mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Nyamira Alice Chae na wengine ambao walisema gavana yuko na uwazi kwa lile alifanya kwa kusimamisha maafisa wake kazi.

“Kwa mwezi mmoja uliopita, sisi kama wabunge tuliona jinsi utumizi wa pesa katika kaunti ya Nyamira ulikuwa mbaya zaidi na tukaenda kumwona gavana ili kujadili hayo, lakini juhudi zetu zikagonga mwamba lakini imefika yeye mwenyewe akajionea kwa macho,” alisema Bosire.

“Tunamuwmba ikiwezekana abadilishe serikali yake na maendeleo yaonekane katika kaunti yetu, sisi tuko pamoja kufanya kazi na gavana wetu maana ameanza kuona yale tuliyokuwa tukimwambia,” aliongezea.

Wakati huo huo, wabunge hao waliahidi kufanya kazi pamoja na kumtaka gavana kwa lolote afanyalo kuwajumuisha wabunge hao ili uongozi wa kaunti hiyo uonekane kuwa kikamilifu.