Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima wa majani chai kutoka eneo la Matunwa, wadi ya Gesima wamewaomba viongozi kutoingiza siasa katika kiwanda kipya cha majani chai kinachotarajiwa kujengwa katika sehemu hiyo.

Wakiongea hii leo, Jumatano katika kituo cha kupimia majani chai cha Riaking’oina –Matunwa, wakulima hao waliwaomba viongozi kuweka siasa kando, kwani wanachohitaji ni kiwanda hicho kama njia ya kuwasaidia wakulima.

Aidha, wakulima hao waliwapongeza wenzao waliokubali na kutoa shamba zao za hekari 12 zitakazotumika kwa ujenzi wa kiwanda hicho.

Kulingana na wakaazi hao, kiwanda hicho ni faida kubwa kwao kwani vijana watapata ajira wakati wa kujengwa na wakati kitaaza kufanya kazi.

“Kuna vijana wetu wengi ambao hawana kazi, tukipata kiwanda hicho, vijana hawa watakuwa na kazi ambayo viongozi hawapi, kwa hivyo tunaomba wenye wako na siasa kwa kiwanda hiki kukoma au kupeleka siasa zao mahali kwingine” alihoji Joseph Moracha, mwenyekiti wa kituo cha Riakingoina

Wakulima hao waliongezea kuwa wako tayari kushirikiana na kiongozi anayeunga mkono mradi wa maendeleo, huku wakimpongeza mwanasiasa victor Ogeto kwa kuwa mtetezi wao kila wakati.