Viongozi wa kisiasa wameshauriwa kuwa waangalifu wanapotoa hotuba yao katika mikutano ya hadhara ili kuepuka matamshi ya uchochezi itakayowagawanya wananchi kwa misingi ya kikabila.
Akizungumza kwenye majengo ya bunge la Kaunti ya Uasin Gishu siku ya Ijumaa, balozi wa amani ambaye pia ni mwakilishi mteule katika bunge hilo, Rose Kisama, alisema ni jambo la kutamausha kuona viongozi wa nyadhifa kuu kama Seneta wa Machakos Johstone Muthama na Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kudaiwa kuchochea umma kwa kutoa matamshi ya uchochezi kwenye mikutano ya hadhara.
Bi kisama aidha alisema kuwa taifa la Kenya li mbioni katika harakati ya uponyanji kufuatia ghasia zilizozuka katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 amabapo maelfu ya watu walipoteza maisha yao huku wengine wakiathirika vibaya.
Kisama aidha aliwataka viongozi kuwacha kumchafulia rais jina na kumtaka Seneta Muthama kumheshimu Rais Uhuru Kenyatta, huku akirejelea matamshi aliyoyatoa katika mkutano wa kutetea haki za walimu jijini Nairobi kuhusu madai ya ufisadi yanayoendelea serikalini.