Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwenyekiti wa muungano wa wanahabari wa ‘Kenya Correspondence Association’ (KPA) William Oloo, amekashifu hatua ya wabunge kupitisha mswada unaozuia wanahabari dhidi ya kufichua maswala nyeti yanayoendelea bungeni.

Kulingana naye, hatua hiyo ni kinyume na katiba ya Kenya.

Akizungunza katika kikao na wanahabari mjini Nakuru siku ya Alhamisi, Oloo alisema kwamba hatua hiyo haijalenga wanahabari pekee ila imewakataza raia kubaini maovu yanayoendelezwa kisiri na wabunge hao.

Alisema kuwa bunge la kitaiafa lingehusisha bunge la seneti katika kupitisha mswada huo.

“Namwomba Rais Uhuru Kenyatta kutotia saini mswada huo na kuurudisha bungeni ili uangaliwe upya na wabunge pamoja na washikadau,” alisema Oloo.

Alisema hayo kwenye shughuli ya kutoa mafunzo inayoendelezwa na Chuo cha Deutsche Welle Academie kwa ushirikiano na Muungano wa wanahabari wa KCA.

Shughuli hiyo ilianza siku ya Jumatatu na itakamilika siku ya Jumamosi.