Baadhi ya wakazi eneo la Kisii wamewaomba waendeshaji bodaboda mjini humo kukoma kutoroka wanapopatikana na kosa.
Wakiongea siku ya Jumanne wakati mwendeshaji bodaboda mmoja aliyefanya kosa la kupitia barabara ambayo bodaboda haziruhusiwi kupitia karibu na Ofisi kuu ya Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae, wakazi hao walioshuhudia kisa hicho waliwakashifu vijana waliona tabia kama hiyo ya kutoroka wakati wamefanya kosa wakisema wanaweza sababisha ajali wanapotimua mbio kukwepa kushikwa.
Kwa sasa wamewaomba vijana hao kuwa wakati kosa limefanyika wanastahili kuitikia sheria kwani makosa ni ya binadamu badala ya kutoroka na kusababisha maafa mengine.
“Nawomba waendeshaji bodaboda kuitikia kosa na kuacha sheria ifuatiliwe iwapo wanapatikana na makosa kwani kutoroka sio jawabu la kudumu kati yao na maafisa wa usalama,” alihoji Bw Kelvin Moindi, mkazi.
Tumekuwa tukishuhudia visa vya waendeshaji bodaboda kufanya makosa na kutoroka, mazoea ambayo yanaweza kusababisha maafa kupitia ajali," alihoji Susan Nyanchama, mkazi.
Kwa upande wa baadhi ya Askari wa Kaunti ya Kisii ambao hawakutaka kutajwa kwa sababu za kiusalama waliwaomba vijana hao kuheshimu sheria za barabara katika mji huo ili kazi iwe rahisi bila kukimbizana kila wakati.