Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafanyakazi kutoka kaunti ya Mombasa ambao walikuwa wakifanya kazi katika timbo la Saruji lililositisha operesheni zake wiki jana baada ya mzozo wa ardhi wameitaka mamlaka ya ushuru ya masuala ya ardhi na mazingira kutoka kaunti ya Kilifi kuharakisha kutafuta suluhu ili wakazi kurejelea shughuli zao za kazi.

Walisema kuwa wamebaki bila kazi tangu timbo hilo kufungwa rasmi na mamlaka ya kaunti ya Kilifi, na kuomba serikali za kaunti zote kutoka eneo zima la pwani kushirikiana na kuleta mwafaka na suluhu la kudumu katika zogo la ardhi ambalo limechangia wakazi wengi kukosa namna ya kujiendeleza katika maisha kiuchumi.

Akiongea Jumapili na mwandishi huyu katika eneo la Majengo mjini Mombasa, mshirikishi wa wafanyakazi hao Chengo Maweu alisema kuwa wengi wa wafanyakazi waliohudumu kwenye timbo lililofungwa hakuwa hata wamelipwa hela zao, na kutoa wito kwa kaunti ya Mombasa na ile ya Kilifi kushirikiana katika kuona kuwa wanapewa haki yao kwa kulipwa.

Chengo alidai kuwa mara nyingi kunapotokea mzozo kati ya serikali na matajiri wao, wafanyakazi ndio huathiriwa sana, na huwa wanajipata katika hali ya kudhulumiwa kwa kunyimwa hela zao na kuzitaka serikali husika kutafuta njia mwafaka kuwapa wafanyakazi fidia ili kuwakimu wakati wapoendelea kutafuta njia mbadala.

“Si haki kwamba tunaumia kwa makosa ya watu binafsi, au ingekuwa shwari serikali kuwa na namna ya kutapa hata mkopo huku tukianzisha hata kama ni biashara ndondogo ili tujimudu, kuliko kuachwa bila njia ya kujitegemea ambapo wengine wetu tuna watoto na familia za kututegemea,” alisema Chengo.