Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanaouza mboga na matunda kandokando mwa barabara kwenye soko la Katito katika Kaunti ya Kisumu wametakiwa kuboresha mazingira katika maeneo wayanouzia.

Akizungumza siku ya Jumatano katika soko hilo, afisa msimamizi wa usafi wa mji kwenye soko hilo, Ambros Odoyo aliwaambia wachuuzi hao kuhakikisha kwamba wanasanya maganda yote ya matunda na kuyatupa katika eneo lililotengwa.

“Kuna sehemu zilizotengwa za kutupa taka. Hivyo basi, mnatakikana kuhakikisha kwamba mnatupa maganda ya matunda baada ya wateja kukula katika maeneno hayo,” alisema Odoyo.

Odoyo pia aliwataka wanaonunua matunda na kuyala papo hapo kutupa maganda na mabaki yanayosalia kwenye mapipa yaliyowekwa na wachuuzi hao.

Aliwataka wasiokuwa na mapipa hayo kutumia vifaa vinginevyo kusanya uchafu pamoja na kisha kutupa kwenye eneo lililotengwa.

Odoyo alisema kuwa hiyo ni njia moja ya kuhakikisha usafi wa mji na kujikinga kutokana na magonjwa yanasababishwa na uchafu kama vile kipindupindu.