Wafanyibiashara katika soko la Gesima lililoko wadi ya Gesima wameiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwajengea vibanda katika soko hilo.
Wakiongea siku ya Jumapili katika soko hilo, wafanyibiashara hao waliomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuwajengea vibanda ili wajikinge kutokana na mvua pamoja na jua kali wakati wa siku za soko.
Wafanyibiashara hao walisema kuwa siku za soko, ambazo ni Alhamisi na Jumapilii wao hutoa ushuru kwa manisipaa ya Nyamira ilhali hawajawai saidiwa na manisipaa hiyo hata kwa kujengewa vibanda.
“Kila siku ya soko huwa tunalipa ushuru kwa manisipaa ya Nyamira lakini cha kushangaza ni kuwa wasimamizi hoa hawajawai tusaidia kujenga soko hili, ili nasi tuweze kufaidika kama wafanyibiashbara,” alisema Prisah Gesimba, mfanyibiashara.
Aidha, walisema kuwa kutokana na soko hilo kuwa mojawapo ya soko kubwa katika wadi hiyo, ni wajibu wa wasimamizi hoa kwawasaidia kujenga vibanda na kukarabati soko hilo.
“Tangu niaze kufanya biashara yangu katika soko hili, sijawahi kosa kulipa ushuru kwa hivyo ni vyema nao kutusaidia ili nasi tuweze kusaidiwa kama wafanyibiashara,” alisema Gesare Oiga, mfanyibiashara.
Wafanybiashara hao walisema wao hupata hasara kutokana na mvua nyingi ambayo inanyesha hasa siku za soko kwa kuwa hawana mahala pa kujingika.
Kwingineko, wamemwomba mwakilishi wao Kennedy Nyameino kupeleka mswaada katika bunge la Kaunti ya Nyamira ambao utawasaidia kushughulikiwa.
“Naomba mwakilishi wetu kutusaidi hata kama ni kupeleka mswada bungeni ili nasi tuweze kukumbukwa,” alisema Evans Ongwenyi.