Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyibishara katika soko la Daraja mbili katika kaunti ya Kisii wameiomba Idara ya Mazingira kutoa ng’ombe aliyesombwa na maji katika mto ulioko karibu na soko hilo.

Wakiongea siku ya Alhamisi katika soko hilo, walisema kuwa ng’ombe huyo alisombwa kutokana na mvua nyingi iliyonyesha siku ya Jumatano.

Kwa sasa wameiomba sekta ya mazingira kuchukua hatua ya haraka na kutoa ng’ombe huyo ambaye ameanza kutoa uvundo katika soko hilo.

Sephania Ongendi mmoja wa wafanyibiashara katika soko hilo alisema kuwa kuna umuhimu kwa tume ya mazingira kuharakisha na kutoa ng’ombe huyo ambaye kwa sasa ameanza kutoa uvundo ambao umewakosesha wafanyibiashara amani ya kuwa katika soko hilo.

“Tunaomba sekta ya mazingira kutusaidia kutoa ng’ombe huyo hapa kwa kuwa hatuna amani kutokana na uvundo ambao unatoka kwa ng’ombe huyo,” alisema Ongendi.

Kwingineko, mhudumu wa afya ya jamii Kepha King’oina amewaomba wenye ng’ombe katika mji huo kuwalinda wanyama hao kwa kuwa wamekuwa wakifariki kiholelaholela jambo ambalo linatishia afya katika kaunti ya Kisii.

“Nawaomba wamiliki wa ng’ombe hawa kuwalinda wanyama hao kwani wakizurura maafa kama haya ndio hutokea na kuharibu mazingira,” alisema Kepha.