Share news tips with us here at Hivisasa

Idadi ya wafungwa wanaofanya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne katika gereza kuu la Naivasha imeshuka mwaka huu na kufikia 17 kutoka 18 mwaka jana.

Kati ya wafungwa wanaojiandaa kuufanya mtihani huo ni pamoja na Solomon Bett, mwenye umri wa miaka 18 na Samson Lenyakopiro mwenye umri wa miaka 45.

Mitihani waliyoratibiwa kufanya wafungwa hao itaanza Alhamisi wiki hii, na licha ya kukumbwa na changamoto kadhaa, watahiniwa hao wameonyesha matumaini ya kufanya vyema wakiwa kizimbani.

Afisa msimamizi wa gereza hilo Patrick Mwenda amesema wafungwa wawili walikuwa wamehukumiwa kifo, huku wengine watatu wanatumikia vifungo vya maisha na wengine wana vifungo vya kawaida.

Kwa mujibu wa afis huyo, idara ya magereza imebuni mbinu mpya ambapo wafungwa wanaofanya vyema wanasamehewa na kuruhusiwa kuungana na familia zao ili waendelee na masomo ya juu.

Kulingana na afisa huyo, hii itakua motisha kwa wafungwa wengi ambao wangependa kuendelea na masomo yao zaidi, na anatumai watafanya vyema kuliko mwaka jana.